Tuesday, September 15, 2009

Hadia Tajik,

Mbunge pekee mwenye

asili ya kigeni, ana miaka 26



Hadia Tajik





Mbunge pekee mwenye asili ya kigeni miongoni mwa wabunge waliochaguliwa jana kwenye uchaguzi mkuu. Hadia amechaguliwa kwa tiketi ya Arbeiderpartiet = AP (Labour Party) kuiwakilisha Oslo Bungeni (Stortinget). AP inawakilisha Oslo na wabunge 6

Amezaliwa Norway tarehe 18 Julai 1983. Anatoka Bjørheimsbygd in Strand, Rogaland

Kabla ya kuchaguliwa, Hadia alikuwa mshauri wa kisiasa wa waziri wa sheria, Bw. Knut Storberget. Aliwahi kushika wadhifa huo kwa waziri mkuu Jens Stoltenberg na pia kwa waziri wa kazi na majumuisho ya jamii Bw. Bjarne Haakon Hanssen.

Amesomea masuala ya haki za binadamu kutoka Kingston University, England na pia ana shahada ya kwanza ya uandishi wa habari toka chuo kikuu cha Stavanger na pia amesomea sheria toka chuo kikuu Oslo.


No comments: