Wednesday, September 16, 2009

Kura mtandaoni

kuanzia mwaka 2011




Karibu Wanorwejiani laki mbili wanatarajiwa kupiga kura mtandaoni kwenye uchaguzi wa mikoa na serikali za mitaa mwaka 2011. Hili litakuwa jaribio na lengo lake ni kujaribu kuongeza idadi ya wapiga kwenye kwenye uchaguzi mkuu wa 2013. Na kuwa hadi uchaguzi wa 2017, Wanorwejiani wote wataweza kukaa majumbani kwao na kupiga kura mtandaoni. Hayo yamesemwa na mkuu wa mradi huo, Bw. Henrik Nore wa Wizara ya Manispaa na serikali za mitaa.

Bw. Georg Apenes, mkurugenzi mkuu wa Idara ya usalama wa masuala ya data (The Data Protection Registrar/Datatilsynet) ameonyesha wasiwasi wake na mradi huo; pale itakapohusu usalama wa kura kwenye mtandao, jinsi kura gani wapiga kura watahakikishiwa usalama wa kura zao.


No comments: