Thursday, September 03, 2009

Roman Abramovich yuko

Tanzania kwa ajili ya

kupanda Kilimanjaro



Roman Arkadyevich Abramovich

Bilionea Mrusi ambaye pia ni mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Arkadyevich Abramovich aliwasili jana usiku kwenye uwanjwa wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, kwa ajili ya kutalii na kupanda mlima wa Kilimanjaro. Aliwasili kwenye ndege yake binafsi ya Boeing 767.

Kwa mujibu wa habari kutoka katika kampuni ya African Environment inayoratibu ziara hiyo, ilieleza baada ya kuwasili alitazamiwa kupelekwa katika hoteli ya River Tree iliyoko Usa River nje kidogo ya mji wa Arusha, kulikuwa na ulinzi mkali kwenye maeneo aliyotarajiwa kufikia.

Tajiri huyo Mrusi alikuwa amepanga kuanza kesho harakati za kupanda Kilimanjaro, na angepiga kambi katika Chuo cha Uhifadhi na Usimamizi wa Utalii cha Mweka kilichoko Moshi mkoani Kilimanjaro.

Abramovich , ambaye aliinunua klabu ya Chelsea mwaka 2003. Amepanga kwenda West Kilimanjaro na kufikia kati ya hoteli za Ndarakwai au Kambi ya Tembo iliyoko West Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro.

Aliweza kumleta kocha stadi, Mreno Jose Mourinho na kusajili nyota kama Didier Drogba, Ricardo Carvalho, Arjen Robben na baadae kuwapa mishahara minono kama Frank Lampard na John Terry na kupelekea timu hiyo kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo katika miaka ya 2004 na 2006 na pia kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka jana, ambapo ilifungwa na Manchester United kwa penati.

Hata hivyo, Abramovich ana sifa pia `ukatili' kutokana na hivi karibuni kuwatimua Mourinho, Adam Grant na Mbrazil Felipe Scolari `Big Phil'.

Chanzo: Nipashe


No comments: