Fujo nchini Gabon
Baada ya Ali Bongo
kutangazwa mshindi
Libreville, Gabon: Serikali ya Gabon imetangaza kuwa mtoto wa marehemu Rais Omar Bongo wa Gabon, ametangazwa kuwa mshindi wa kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu wa Rais.
Fujo zimeanza kwenye mji wa Port Gentil, baada ya watu kupinga kutangazwa kwa waziri wa ulinzi, Ali Bongo kama mshindi wa Urais kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika hivi majuzi.
Mjini Libreville, polisi ilibidi kufyatua mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji, huku kiongozi mkuu wa upinzani, Pierre Mamboundou kaingia mafichoni.
Mjini Dakar, Senegal, waandamanaji walivamia ubalozi wa Gabon na kuuchoma moto.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amewaomba Wagaboni kuwa watulivu na kusisitiza wagombeaji wa Urais kutatua hitilafu za uchaguzi huo kwa njia za amani na kibin-adam.
Familia ya marehemu Omar Bongo inamiliki majumba kama 45 nchini Ufaransa na biashara nyingi nyingi ndani na nje ya Gabon. Gabon nchi yenye mafuta, lakini watu wake bado ni maskini sana. Gabon wanazalisha mapipa 247,000 ya petroli kila siku, kufuatia na taarifa za wizara ya nishati ya Marekani, (US Energy Administration)
No comments:
Post a Comment