Serikali yawasikiliza wanafunzi
wa sekondari ya Kibasila
Hatimaye serikali imesikia kilio cha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Kibasila jijini Dar es Salaam kwa kuagiza kuwekwa matuta katika barabara ya Mandela na Chang'ombe kwenye makutano ya barabara hizo jirani na kiwanda cha Bia cha Serengeti. Hali hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya wanafunzi wa shule hizo kukaa barabarani kwa saa tano wakiishinikiza serikali kuweka matuta baada ya wanafunzi watatu kugongwa kwa siku tofauti kutokana na mwendo kasi wa magari yanayotumia barabara hiyo kutozingatia usalama wao
Akizungumza na baadhi ya wanafunzi hao katika eneo la tukio leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi amesema kuwa, yeye binafis amesikitishwa na kitendo cha madereva ambao wasiojali usalama wa watu wanaotumia barabara hiyo hasa watembe kwa miguu na badala yake wao hutumia kama ni yao pekee. Mh. Lukuvi ameitaka sekta husika kuhakikisha wanaweka matuta kabla ya wiki hii kumalizika kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
VIDEO NA: ISMAIL MANG'OLA/ Global Publishers Limited
No comments:
Post a Comment