Ukifanya haya uhusiano
wako utadumu!
HABARI za leo wapenzi wasomaji wangu,mambo vipi? mko poa? Kwa upande wangu mi niko safi na kama ilivyo ada nakuletea vitu muhimu vitakavyodumisha uhusiano wako.
Jamani eeh nasema hivi hapa duniani hakuna mnyama mgumukumlisha kumlindana na kumuhudumia kama mahusiano mmenipata, Wanakwetu?.
Hakuna hata uhusiano mmoja ulioweza kudumu bila mikwaruzo na hii ndio sababu wahenga walisema vikombe kabatini haviachi kugongana ikiwa ni miongoni mwa maneno ya busara zaidi katika kukuza mahusiano.
Kwa kuwa ukubwa ni jaa, mi sioni shida kuwapa ‘tips’ muhimu sana katikakudumishauhusiano wako na yule wako hususani wa ubani.
Pigania penzi lako
Ninaposema kupigania simaanishi kwa mishalena mikuki la hasha! Namaanisha kutumia muda wakokatika kuhakikisha umpendaye anakuwa wako siku zote.
Unachotakiwa kufanya ni kuwa na mpangilio katika shughuli zako za kila siku kama ujuavyo mwanamke shughuli babu …! umia maufundi yako yote katika kwenda sawa katika hili.
Epuka mabishano yasiyo ya lazima
Katika mahusiano suala la majibizano hasa yale ya ugomvi hupelekea mifarakano, hivyo haipendezi wala haileti maana katika kujenga uhusino makini.
Nasema hivi siku zote wanawake wanakuwa mahodari wa kuchonga ,…! Ikiwa kweli unahiataji kudumisha uhusiano wako achana na tabia hii kwani itakukost.
Tambua msamaha wa mwenzio
Makosa ni jambo la kawaida katika mahusianao la msingi ni kuhakikisha kuwa endapo makosa yatatokea na mwenzio akajirudi na kuomba msamaha, hakikisha unamsamehe kwani hakuna aliyekamilika
Elewa sisi ni watu na si malaika kwa kutambua maana na thamani ya msamaha, itasaidia sana kuweka uhusiano wenu katika hali nzuri, upo hapo shost.
Mahaba!mahaba! mahaba!
Hakuna mazoea katika uhusiano wa mapenzi jitahidi kuwa mbunifu katika kuboresha mahusino yenu.
Mfanye umpendaye ajione wa kipekee na pia hakikisha huduma zako zinakuwa unique mwanamke mipangilio………... umenielewa mwanakwetu. Ni vizuri kuelewa kula uhondo, kwataka matendo na pasipo mateneo utaambulia uvundo …! Kuwa mwangalifu shost!.
Acha kicheko kitawale
Kicheko ni tiba nzuri sana ya kiroho, kwani husaidia sana katika kukujenga kisaikolojia na pia kuupa sura uhusiano wako.
Kisirani hakina nafasi katika ujenzi au udumishaji wa mahusiano, hivyo ikiwa unataka kudumisha uhusiano wako hakikisha kicheko kinakuwa sehemu ya maisha yako.
Kuwa mwenyewe! usiigize
Jamani hakuna maigizo katika mapenzi kamwe usijifekishe, kuwa mwenyewe siku zote itakusaidia kumfanya umpendaye akuamini, ajivunie kuwa na wewe.
Kujifekisha kwako kutakudharaulisha, kuwa makini babu, wewe ni wewe na hakuna atakayefanana na wewe maisha shost!
No comments:
Post a Comment