Siku ya mwisho ya kampeni
za uchaguzi mkuu hapa
Norway.
Leo ni siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi mkuu hapa Norway. Kwenye mtaa mkuu hapa Oslo wa Karl Johan, vibanda vya kampeni vya vyama tofauti viko bega kwa bega. Hakuna kutupiana maneno machafu, kushikana mashati wala kuchapana bakora na mijeledi. Kila chama kinajaribu kunadi sera zake kwa kiustaarabu!!
Bunge la Norway, Stortinget
Kibanda cha Liberal Party (Venstre)
Ja vi kan (Kinorwejiani) for Yes We Can.
Tangazo la Baraza la muungano wa vyama vya kijamii vya wahamiaji (Rådet for innvandrere i Oslo) lililo chini ya Manispaa ya Oslo. Tangazo linahimiza wageni walio na haki ya kupiga kura kutumia nafasi yao kesho kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Kibanda cha Labour Party (Arbeiderpartiet) kiko bega kwa bega na kibanda cha Progress Party (Fremskrittspartiet) Vyama hivi ndivyo vyama vyenye upinzani mkali na itikadi tofauti kabisa inapohusu jinsi gari watasukuma gurudumu la maisha hapa Norway.
Kibanda cha Progress Party (Fremskrittspartiet kifupi FrP)
Kibanda cha Socialist Left (Sosialistisk Venstreparti)
Kibanda cha Christian Democratic Party (Kristelig Folkeparti kifupi KrF)
Kibanda cha the Conservative (Høyre kifupi H)
Kibanda cha RED au RØDT (ROEDT)
Kibanda cha chama cha Waliostahafu (Pensjonistspartiet)
Gari linaloendeshwa na nishati rafiki ya mazingira la Agrarian Party (Senterpartiet)
No comments:
Post a Comment