Victoria Rweikiza agombea
Ubunge Jumatatu 14th Sept.
Dada Victoria Rweikiza, mwenye asili ya Tanzania anagombea ubunge kupitia chama cha ”RED au kwa Kinorwejiani RØDT (bofya na angalia tovuti yao). Bi. Victoria ni wa nne kwenye orodha ya wagombea wa RED wa Oslo. Kama wakipata asilimia kati ya 6 na 8 nchi nzima, Bi. Victoria anaweza kuwa Mbunge.
Hapa Norway, chama chochote kinawakilishwa Bungeni kutokana na asilimia ya kura kitakachopata. Hii inatokana na kuwa wana mfumo wa uwakilishi wa uwiano ( proportional representation). Ina maana jimbo moja linawakilishwa na zaidi ya mtu mmoja, kutokana na wingi wa wakazi wanaokaa jimbo hilo. Hivyo kama hapa Oslo kuna wa 578 870 (takwimu za Aprili Mosi, 2009), jimbo la Oslo lina nafasi za wabunge 17 jumla
Arbeiderpartiet (The Labour Party) wabunge 6
Hoeyre (The Conservative) wabunge 3
Fremskrittspartiet (The Progress Party) wabunge 3
Socialist Left (SV) wabune 2
Liberal (Venstre) wabunge 2
Christian Democratic Party (KrF) mbunge 1
(Takwimu hii ni ya uchaguzi wa 2005).
Kila chama kinapendekeza watu wake kuanzia wawili hadi 25, kwa kila jimbo. Wingi wa kura kitaifa ndio unaamua wabunge wangapi wa chama flani ndio watawakilisha chama chaoBungeni (Stortinget). Mwaka 1989, ilipitishwa sheria kuwa, chama kikipata 4% ya jumla ya kura nchi nzima, basi kinapata nafasi ya kuwakilishwa na wabunge wawili.
Bofya na soma zaidi kuhusu uchaguzi mkuu hapa Norway mwaka 2009
Tumtakie Bi. Rweikiza kila la heri Jumatatu 14.Septemba 2009 siku ya uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment