Monday, September 28, 2009


Watu 6 wakamatwa

kwenye wizi wa kikomandoo

uliofanyika Stockholm



Hapa majambazi walipotua na helikopta juu ya paa la ghala la kuhifadhia fedha. Walivunja kioo (mkono wa kushoto) na kuingia kama makomandoo ndani na kulifti magunia ya hela na helikopta na kuondoka huku polisi wakiwa wameduwaa.


Jumla ya watu sita wamekamatwa mjini Stockholm, kufuatilia wizi wa kikomandoo kwenye ghala la fedha uliofanyika Jumatano iliyopita mjini Stockholm, limetangaza shirika la habari la Sweden; Tidningarnas Telegrambyrå (TT). Mtu mmoja mwenye miaka 34, anayesadikiwa kuwa ndiye alikuwa rubani wa helikopta iliyotumika kwenye wizi huo, naye amekamatwa. Tayari jamaa huyo ameshaomba atetewe na wakili mmoja supastaa nchini Sweden, Bw. Leif Silbersky.

Gazeti la Express (Sweden) limeandika kuwa; majambazi hayo yamekamatwa na tiketi za ndege za kuelekea kwenye nchi za Asia. Walikuwa waondoke kuelekea kwenye hizo nchi jana. Mmoja kati ya hao sita, alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Stockholm wa Arlanda.

Wizi huo uliofanywa kwa staili ya kikomandoo, uliwaacha polisi wa Sweden mdomo wazi, kwani hawajawahi kushuhudia ujambazi wa namna hiyo. Inasadikiwa kuwa wengi wa majambazi hayo; walikuwa makomandoo kwenye vikosi maalumu vya kikomandoo kwenye Jamhuri ya Yugoslavia iliyovunjika.


No comments: