Daktari mpasuaji akamatwa
baada ya miaka 5
Mark Weinberger alyechuchuma kwenye hema. 15. Desemba 2009 alikamatwa na polisi.
Daktari mpasuaji Mmarekani Mark Weinberger (46) amekuwa akitafutwa kwenye kipindi cha Americas Most Wanted na FBI na idara zingine za usalama za Marekani kwa miaka mitano sasa, amekamatwa akiwa kwenye hema kwenye mlima mrefu kuliko yote Ulaya Mont Blanc, ulioko kwenye milima ya Alpe.
Daktari bingwa huyo mpasuji wa koo na pua, amekuwa akiishi kwa kula vyakula vya makopo na maji ya kuyeyusha kutoka kwenye theluji na barafu.
Kabla ya kuwakacha FBI, Mark Weinberger alijipatia utajiri wa haraka haraka kwa kufanya upasuaji wa kuwasawazisha watu sehemu za miili yao ionekane vizuri (Upasuaji wa plastiki) kwenye kliniki yake binafsi (Weinberger Sinus Clinic). Jamaa alikuwa anachuma Dala za Kimarekani 200 000 (laki mbili) kwa wiki (Kroner milioni moja na pointi 2 hivi/Tshs. 271,938,880.00).
Mwaka 2002 alishtakiwa na dada mmoja kwa sababu alimfanyia upasuaji wa plastiki huku akijua kuwa huyo dada alikuwa na saratani (kansa). Baadaye watu 25 wakajitokeza kumshtaki daktari huyo kwa makosa aliyowafanyia, alipowatengeza miili yao.
21. Desemba 2004 mkewe Mark, Michelle aliamka na kukuta mumewe hayupo kitandani. Alipoangalia ndani ya nyumba, akakuta mumewe kachukua hela na pasipoti na jii amepotea!
Polisi walitonywa na wapanda milima ya Alpe juu ya mtu waliyehisi si mpanda milima bali anaishi milimani. Sehemu aliyokutwa na kukamatwa halibaridi huwa inashuka hadi kufikia -20 chini ya nyuzi za baridi. Mark amelazwa kwenye hospitali ya Molinette mjini Torino, Italia.
Tayari amejaribu kujiua chooni kwenye hospitali hiyo, akawahiwa. Watu karibu 200 wamemshtaki jamaa huyo hadi sasa.
No comments:
Post a Comment