Jua leo limetoka
Halibaridi –16o C !!!
Baada ya siku kadhaa kupotea, leo asubuhi hadi adhuhuri jua limetoka. Kuamkia leo kulikuwa na baridi kali na halibaridi ilikuwa kutoka -16o C hadi -20o C baadhi ya sehemu za mashariki ya Norway, ikiwemo Oslo. Watu walipata shida kuwasha magari yao asubuhi. Barafu ilikuwa imeganda kwenye magari.
Watu wengi wako likizo ya Krismasi hadi Januari 3. Wengi wenye watoto wametumia siku ya leo, kwenda kucheza michezo ya kuteleza kwenye theluji, kama inavyoonyesha picha hapo juu.
Utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuwa halibaridi itazidi kushuka chini kufikia -20o C. Watu wanashauriwa kuamka mapema ili wapate muda wa kuwasha magari yao kabla ya kwenda kwenye mihangaiko. Wanashauriwa pia kuendesha kwa makini na uvumilivu!
No comments:
Post a Comment