KIPENZI CHETU SIMBA WA VITA MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA HATUNAYE TENA. MZEE KAWAWA AMETUTOKA LEO ASUBUHI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOLAZWA TOKEA JANA BAADA YA KUPATA MATATIZO YA KIAFYA. ALIZALIWA LIWALE MWAKA 1926 AMBAPO BAADA YA KUSHIKA NYADHIFA MBALI MBALI ALIKUWA WAZIRI MKUU KUANZIA JANUARI 22, 1962 HADI FEBRUARI 13, 1977 AKIFUATIWA NA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE. BAADAYE ALIKUWA KATIBU MKUU WA CCM KABLA YA KUSTAAFU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ametangaza siku saba za maombolezo kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mzee Rashid Mfaume Kawawa, aliyefariki duania leo saa 3:20 asubuhi baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu kwa muda huo bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti.
Rais alisema kuwa taratibu zote mazishi zitasimamiwa na serikali na atapewa heshima kwa muasisi wa kupigania uhuru wa Tanzania.
Mwenyezi Mungu Amweke Pema. Ameen!
No comments:
Post a Comment