Obama atakuwa
siku mbili Oslo

Rais Barack Obama anatarajiwa kuja mjini Oslo Alhamisi Desemba 9, kwa minajili ya kupokea tuzo ya amani ya Nobel, Ijumaa Desemba 10. Rais Obama na ujumbe wake watafikia hoteli ya Grand kati kati ya Oslo kwenye mtaa mmoja maarufu wa Karl Johan. Hoteli yote imekodishwa siku hizo kwa ajili ya ujumbe utakaoongozana na Rais Obama.
Lakini ratiba ya kufika kwa Obama inaweza kubadilika wakati wowote. Imekuwa ikibadilika toka alipokubali kuja kupokea tuzo hiyo. Ulinzi mkali umeshaanza kuonekana mjini Oslo siku kadhaa sasa, jamaa wa Secret Service wameshamwagwa Oslo, wakisaidiwa na jamaa wa usalama wa taifa wa Norway
Mashimo ya maji machafu mjini Oslo kuzungunguka maeneo anayotarajiwa kupita Obama, yamepigwa ”welding”. Watu wanaofanya kazi karibu na maeneo hayo wamefanyiwa uchunguzi wa kina na polisi. Maduka yanayozunguka Hoteli ya Grand yatafungwa kwa siku hizo, watu wanaofanya kazi kwenye maofisi ya karibu na wale wanaokaa kwenye maorofa ya karibu wameonywa kutochungulia madirishani siku hizo, Obama atakapokuwa mjini Oslo.
Jeshi la anga la Norway limeashiria kuwa ndege zake za kivita zitaonekana zikiruka kwenye maeneo ya Oslo, watu wasiogope.
Kwa tahadhari: Ukitembea mjini Oslo tembea na kitambulisho chako, usishangae ukisimamishwa na kuulizwa kitambulisho!
No comments:
Post a Comment