Sunday, December 06, 2009

Watu 30 wavamiwa na

Polisi na kurudishwa

kwao kuamkia leo



Saa 7 za usiku wa manane kuamkia leo, polisi imevamia nyumba kadhaa mjini Oslo na kuwakamata Wairaki 30 walionyimwa hifadhi za kikimbizi. Wanaume hao wamerudishwa Baghdad na ndege maalumu iliyokodishwa na kitengo maalumu cha polisi kinachoshughulikia wageni (Politiets utlendingsenhet). Karibu polisi 60 walikuwemo kwenye msafara huo wa kuwarudisha Wairaki hao.

Kwa kuhofia kuwa jamaa wangetonywa juu ya msako huo, polisi waliifanya operesheni hiyo kwa siri kubwa.

Chanzo cha habari: TV2 nyhetene


No comments: