Sunday, January 10, 2010

Angola wavurunda dakika 11 za mwisho!





Timu ya taifa ya Angola, Palancas Negras (The Black Antelopes) imeanza kwa kuvurunda kwenye ufunguzi wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika, baada ya kutoka sare na Mali, Les Aigles (The Eagles) kwa mabao 4 – 4 kwenye uwanja wa Estádio 11 de Novembro mjini Luanda. Angola wakicheza mbele ya Rais wao Jose Eduardo dos Santos, walikuwa wanaongoza kwa magoli 4 – 0 hadi kwenye dakika ya 79. Mali walisawazisha magoli 4 kwa kipindi cha dakika 11 za mwisho wa mpira!!

Wakati huo huo, timu ya taifa ya Togo imerudi nyumbani lakini waziri wa michezo wa nchi hiyo, ameliomba shirikisho la soka la Afrika CAF kuwa timu yao imepewe muda wa siku tatu wa maombolezo, halafu waruhusiwe kurudi na kuendelea na mashindano. Mpaka sasa CAF haijatoa tamko lolote juu ya ombi hilo la Togo.

No comments: