Sunday, January 03, 2010

Ni rahisi simu na SMS zako kusikilizwa


Kwenye kongamano la Chaos Communication Conference hivi karibuni mjini Berlin, mtafiti mmoja wa Kijerumani aitwaye Karsten Nohl amevunja koda (code) iliyodumu miaka 20 ya simu za mkononi zinazotumika karibu duniani za GSM. Amevunja koda hiyo kwa kutumia program ya dezo.  Amesema kuwa kosa la GSM liko kwenye namna moja ya hisabati inayotumika na makampuni ya simu iitwayo A5/1.

Alichofanya Nohl ni kuchukua kompyuta yenye Terabyte 2 na jedwali liitwalo "Cracking" linalotumika kutafuta "funguo ya kufungua koda" na ambalo hutumika kuhakikisha usalama wa simu na wa jumbe fupi (SMS).

Kwa kutumia Terabyte 2, "cracking", program maalumu na kompyuta vyote vikiwa na gharama za Kroner 150 000 (lakimoja) za Kinorweji, mtu yeyote anaweza kusikiliza simu za mkononi na kusoma SMS ya simu yoyote ile.

Inajulikana kuwa tayari vyombo vingi vya usalama na dola vya nchi duniani vina vifaa hivyo vya kusikiliza na kusoma SMS.

Msemaji wa shirikisho la GSM amesema kuwa wanachunguza hilo na tayari wameshatengeza  hisabati ingine iitwayo A5/2 ambayo ni vigumu kuivunja na ambayo inatumika kwenye simu za 3G.

3 comments:

Mosi_o said...

Tuwe tu waangalifu na makini tunapozungumza kwenye simu za mkononi na tunapotuma SMS

Mosi_o said...

Tuwe tu waangalifu na makini tunapozungumza kwenye simu za mkononi na tunapotuma SMS

Mosi-O-Tunya said...

Tuwe tu waangalifu na makini tunapozungumza kwenye simu za mkononi na tunapotuma SMS...

Niliponyokwa na vidole kama wasemavyo Waswahili ndo´maana zimetoka jumbe tatu kutoka kwangu