Saturday, January 09, 2010


Wanajua pesa ni sabuni ya roho, kumbe ni mkaa wa uroho maana unawachafua mwisho


Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.



Heri ya mwaka mpya mpenzi wangu,


KWA mara nyingine nasherehekea (nasherehekea???) Mwaka Mpya bila kuwa na mpenzi wangu. Siku zinazidi kwenda na kama mwaka jana na juzi nakaa na kumwomba Mungu mwaka huu uwe mwaka wa mwisho wa sisi kukaa mbalimbali hivyo.


Namwomba Mungu biashara yako ifanikiwe tuweze kukaa pamoja kama mume na mke, tuweze kusaidiana kujenga maisha kwa pamoja. Mara nyingine namwomba Mungu hata bosi ashindwe katika uchafuzi ujao ili nilazimike kurudi nyumbani. Mpenzi wangu najua wataka tuwe na maisha ya raha, lakini mimi sina shida na dhiki. Tunaweza kula ugali na mbilimbi mwaka mzima ili mradi niko na wewe. Kukaa mbali na wewe hiyo ni dhiki tosha kwanza......bofya na endelea>>>>>

No comments: