Friday, April 16, 2010


Kufungwa kwa anga la Norway:
John Cleese achukua taxi toka
Horten, Norway hadi Ubelgiji

John Cleese alipokuwa kwenye kipindi cha Skavlan, NRK jana jioni.

Kufungwa kwa anga la Norway jana na leo kumewaathiri wasafiri wengi. Waziri mkuu wa Norway Jens Stoltenberg alikwama New York kwa siku moja alikoenda kuhudhuria mkutano wa usalama wa nyuklia aliotishwa na Rais Obama. Mpaka makala hii inaandikwa Stoltenberg alikuwa amefika Madrid, Hispania.

Walio na hela kama mchekeshaji Mwingireza, John Cleese hadithi ni nyingine.  Cleese alikuwa Norway kwenye safari ya kikazi na leo aliamua kuchukua taxi tokea Horten (Norway) hadi Brussels (Ubelgiji), safari ya masaa 14 hadi 16. Mpaka walipofika Gothenburg (Sweden) gharama za taxi zilikuwa kroner 30 000,- kama Dola za Kimarekani 5114,- (T.shs. 6,868,102.00) Sijui gharama zitafikia kroner ngapi hadi watakapofika Brussels.

No comments: