Friday, April 16, 2010

Kunani Afrika Mashariki, mbona kila nchi inajizatiti?

Uganda kununua
Sukhoi Su-30 MK2 Jet Fighters
SU-30 MK2 ya jeshi la anga la Venezuela.





Inasadikiwa kuwa Uganda imetia mkataba na Rosoboronexport, kampuni ya taifa ua Urusi ya uuzaji wa silaha za kivita. Uganda inatarajiwa kupokea ndege sita za kivita za aina ya Sukhoi SU-30 MK 2 kwa gharama ya shilingi za Uganda bilioni 108 kila moja. Pia kampuni hiyo itaiuzia Algeria ndege 16 za aina hiyo. Habari hizi zimeripotiwa na Vedomosti la nchini Urusi.

Msemaji wa jeshi la wananchi wa Uganda (UPDF), Luteni Kanali Felix Kulayigye, amekanusha ununuzi huo wa Sukhoi na badala yake amesema kuwa Uganda wamepeleka ndege zake za kivita za aina ya MiG-21 “Fishbed” kwenye kampuni hiyo ya Rosoboronexport kwa kuziunda upya. Lt.Kanali Kulayigye alikubali kuwa kweli Uganda ilifanya mazungumzo na kampuni hiyo, lakini ilijitoa kwenye mazungumzo ya kununua ndege hizo za kivita kwa sababu ya gharama zake.

Kama Uganda kweli wakizipata ndege hizo sita za kivita, basi Uganda itakuwa na moja ya jeshi la anga lenye ndege za kisasa nchini Afrika. Itakuwa tishio kwa nchi za Afrika Mashariki, kwani Kenya na Tanzania zina ndege za kivita zilizobuniwa miaka 50 iliyopita.

Sukhoi SU-30, inajulikana kama Flanker kwa nchi za NATO, ziko modeli mbali mbali. Iliingia kwenye jeshi la anga la Urusi mwaka 1996. Ina kasi ya Mach 2.0 (2,120 km/h, 1,320 mph) na ni ya kisasa au kwa msemo mwingine ni “4.5 Generation of Fighter Jets”. Flanker inafananishwa na Eurofighter Typhoon na F-15E Strike Eagle ya Marekani. 


Nchi ambazo zinatumia SU-30 MK ni Algeria, Uchina, India, Indonesia, Malaysia, Urusi, Uganda, Venezuela, Vietnam.

Tanbihi:

Kuna nini Afrika Mashariki? Hivi majuzi Kenya walinunua ndege kutoka jeshi la anga la Jordan, japo zimetumika na za zamani. Uganda wanajibu mapigo kwa kununua ndege za kisasa. Je, wanajitayarisha kwa vita? Sisi Tanzania na ndege zetu MiG-19 na MiG-21 tutawamudu Waganda? Hizo MiG zetu hazitafua dafu hata kwa nini....Sukhoi SU-30 Flanker moto wa kuotea mbali. Nimeziona kwenye maonyesho ya ndege wakati flani hapa Norway, ni hatari. Ndege za kivita za familia ya Sukhoi-27, Sukhoi-30, Sukhoi-33 na kuendelea, ndizo pekee za kivita zinazoweza kwenda kwa mwondoko unaoitwa ”Cobra manouvre”

Chanzo cha habari hizi:
  1. Vedomosti la nchini Urusi.
  2. http://en.wikipedia.org/wiki/Sukhoi_Su-30

6 comments:

Anonymous said...

Wee acha tu Waganda watakuwa wanafanyia mazoezi kwenye anga la Tanzania bila sisi kufanya lolote...

Anonymous said...

Tanzania itaishia kununua ndege za kivita toka China zilizotengenezwa kwa leseni toka Urusi

Anonymous said...

Museveni anatakakutawala Afrika Mashariki. Hayo ni matayarisho ya mwanzo. Yakikamilika .... Booom kaingia Bukoba,Mwanza. Natarajia Tanzania nao wako katika matayarisho kimya kimya. Hiyo ndio kazi kubwa ya TISS = Tanzania Intelligence

Anonymous said...

Kazi hiyo ni TISS kuhakikisha Usalama wa Watanzania. Lakini si unajua tena TISS wanavyopeana kazi kinduguwengine hawakocompetent kabisa kazi yao kujitangaza oh..,mimi usalama wa taifa ili watu wamwogope...

Anonymous said...

Jamani kama hamjui, inapokuja kwenye usalama wa taifa, Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika. Tanzania Intelligence & Security Service (TISS) wana uwezo mkubwa sana na wana vijana wengi wanaojua kufanya kazi, achilia mbali hao wanazunguka mitaani na kujitangaza!!!!

Anonymous said...

Waganda watakuwa na advantage kwani Sukhoi-30 ni all weather fighter jet, wakati MiG-19 na MiG-21 haziwezi kuruka kama kuna mvua au mawingu mengi, hapo tu peke yake tumeshindwa. Bila hata kugusa ubora wa hizo ndege.

Kama kawaida ya Tanzania, sidhani tuko kimya. TISS tayari watakuwa wamejua ununuzi wa Waganda muda mrefu kabla ya sisi watu wa kawaida kujua.

Ndio moja ya kazi yao.

Na tayari watakuwa wametoa taarifa kwenye military intelligence ya JWTZ au vice versa.

Tupo imara!!!