Wednesday, April 21, 2010


Serikali ya Ufaransa kupiga
marufuku niqab na burka


Serikali ya Rais Nicolas Sarkozy itapeleka muswada kwenye bunge la Ufaransa mwezi Mei wa kupiga marufuku uvaaji wa Niqab na Burka kwenye sehemu zote za umma.  Luc Chatel, msemaji wa Rais Sarkozy amesema kuwa; uamuzi huo wa serikali ya Ufaransa ulifikiwa kwenye mkutano wa baraza la mawaziri. Wachunguzi wa mambo wanasema kuwa muswada unaungwa mkono na wabunge wengi, hivyo ni wazi kuwa utapita na kuwa sheria.

No comments: