Friday, April 30, 2010



Ubelgiji yapiga marufuku mabaibui
kwenye sehemu za umma


Bunge la Ubelgiji jana lilipiga kura na kupitisha sheria ya kupiga marufuku uvaaji wa Niqab na Burka (mabaibui) kwenye sehemu za umma. Wabunge 136 walisema NDIYO na wawili walikataa kupiga kura.

Kukiuka sheria hiyo, mtu anaweza kupigwa faini kati ya Euro 15 hadi 25 (sawa na kroner za Kinorwejiani 118-196 au shilingi za Tanzania 26956.50 hadi 44927.50) au jela siku saba au faini na jela pamoja.




No comments: