Waombaji ukimbizi kwa utaifa
Kuna mdau mmoja msomaji wa blogu hii ameomba tafsiri ya ”Asylum application by nationality” kwa Kiswahili. Ifuatayo hapo chini ni tafsiri ya mhariri. Mhariri anaomba kumradhi kama tafsiri hii haijitoshelezi. Takwimu zilizopo kwenye hivyo viungo hapo chini ni idadi ya waombaji na nchi walizotoka. Ni matumaini kuwa halitakuwa tatizo kubwa kwa aliyeomba itafsiriwe kwa Kiswahili.
********************************************
Mwombaji ukimbizi ni mtu ambaye kwa hiari yake mwenyewe kaja na kuomba hifadhi hapa Norway. Kwa mujibu wa kanuni za haki za wakimbizi za Umoja wa Mataifa za mwaka 1951 na sheria za nchi hii, Norway inawajibika kuwalinda wote ambao kwa sababu za imani zao za kidini, utaifa, itikadi za kisiasa au kuwa mwanachama wa kundi la kijamii linaloonewa, kuamua kukimbia na kuja kuomba hifadhi ya ukimbizi.
Bofya na fungua viungo hapo chini – orodha ya watu kutoka nchi mbalimbali walioomba hifadhi:
- waombaji kwa utaifa 2010, 1.Januar-31.Machi.
- waombaji kwa utaifa mwaka 2009
- waombaji kwa utaifa mwaka 2008
- waombaji kwa utaifa mwaka 2000 hadi 2008
1 comment:
Shukrani sana sana tena sana kwa kukubali ombilangu la kuniandikia kwa lugha ya nyumbani ubarikiwe sana kazi njema
Post a Comment