Thursday, April 15, 2010

Usafiri wa anga Norway wasimamishwa

Wasafiri waliokwama kwenye uwanja wa ndege wa Gardemoen Oslo leo.


Kuanzia saa 4 leo usafiri wa anga kutoka na kuingia Norway umesimamishwa. Sababu kubwa ya kusimamishwa ni wingu kubwa kutanda sehemu kubwa ya anga la Ulaya ya Kaskazini kufuatilia volkano iliyolipuka nchini Iceland hivi majuzi. Iceland imekumbwa na balaa la kulipukiwa na volkano kubwa kwa kipindi kisichozidi mwezi.

Idara ya usafiri wa anga ya Norway, Avinor imesema, kufungwa kwa anga ya Norway na kusimamisha usafiri wa anga kutawaathiri wasafiri kati ya 70000 hadi 100000. Avinor wamesema huenda na kesho pia anga ikafungwa.

Chanzo: Avinor

No comments: