Wednesday, May 26, 2010


Idara ya uhamiaji kuwapa vibali vya
kazi wasio na makaratasi


Idara ya uhamiaji hapa Norway, Utlendingsdirektoratet (UDI), imependekeza kwa serikali kuwa waombaji wasio na uthibitisho walikotoka na ambao wameomba hifadhi ya kuishi Norway, wapewe vibali vya kufanya kazi, endapo UDI na polisi watatumia zaidi ya miezi 3 kushughulikia maombi ya waombaji. Na kuwa ni wajibu wa mwombaji kutoa taarifa kwa mwajiri wake, atakapokataliwa kuishi hapa na kuambiwa aondoke.

Mapendekezo hayo ya UDI, yamepingwa vikali na polisi na Jumuiya wa waajiri wa Norway, Confederation of Norwegian Enterprise (NHO)

Polisi na NHO, wanadai kuwa itakuwa ni kichekesho kwa mtu ambaye taifa halijui anatoka wapi na amekuja Norway kwa minajili gani, anapewa kibali cha kufanya kazi hivi hivi tu. Wametoa sababu kadhaa za kupinga waombaji wasio na vitambulisho walikotoka wasipewe vibali vya kufanya kazi:

  • Itakuwa kichekesho kwa mtu kukataliwa kuishi hapa, halafu eti aende mwenyewe na kumweleza mwajiri wake kuwa ameambiwa aondoke. Mtu atakaa kimya na huku akiendelea kufanya kazi, bila ya kuchukuliwa hatua yoyote.
  • Kwa usalama wa nchi; lazima polisi waelewe asili ya wote wanaoishi na kufanya kazi hapa. Isije Norway ikawa peponi kwa mafisadi, magaidi na wahalifu  na itarahisisha kazi ya polisi hapo baadaye mtu huyu atakapoomba uraia, kwani masharti ya kuomba uraia yana vipengele vingi vya kubabaisha. Mtu huyu akioa/akiolewa na kukaa hapa zaidi ya miaka 7 anaweza kuomba uraia na itakuwa vigumu kumkatalia.

No comments: