Rais Umaru Yar´dua afariki dunia
Rais Umaru Yar´adua amefariki dunia jana akiwa na miaka 58 baada ya kuugua kwa mrefu. Yar´adua amekuwa akiugua tokea Novemba mwaka jana na hajaonekana hadharani toka wakati huo. Alilazwa hospitalini nchini Saudi Arabi hadi Februari aliporudi Naijeria kimya kimya.
Kaimu Rais (Makamu wa Rais) wa Naijeria, Goodluck Jonathan, atashikilia madaraka hadi uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwakani.
Yar´adu ni Rais wa kwanza wa Naijeria mwenye elimu ya chuo kikuu toka nchi hiyo ipate uhuru wake mwaka 1960. Alikuwa na shahada ya uzamili ya sayansi toka chuo kikuu cha Ahmadu Bello, aliyoipata mwaka 1980.
No comments:
Post a Comment