Monday, May 10, 2010

Norway

Waafrika mazezeta!



Mtafiti wa TEKNOHAMA na mwandishi, Ole Jørgen Anfindsen (pichani) anasema kuwa Waafrika wana akili ndogo (IQ = intelligence quotient) kuliko watu wengine duniani. Amesema wazi leo kwenye kipindi cha “TV 2 alltid nyheter” saa 18:55 – 19:19 CET, kuwa kwa kuwa watu wa mataifa mengine akili zao ni finyu, basi ni vigumu watu kutoka mataifa hayo, kuzoea mila, desturi na utamaduni wa Norway, hususan wa nchi za magharibi. Akiendelea, alisema kuwa watu wenye IQ ndogo inakuwa vigumu kuenda sambamba na teknolojia inavyoenda kasi.

Alikuwa akielezea utafiti alioufanya na kuandika kwenye kitabu chake kiitwacho “Selvmordsparadigmet”. Pamoja na kuelezea uzezeta wa Waafrika, pia ameishambulia siasa na sheria za zinazohusu wageni kuwa ni laini mno kiasi cha kutia aibu. Anapendekeza sheria za wageni kuzibwa matundu na kukazwa zaidi ili wageni wasiingie Norway kiholela.


3 comments:

Anonymous said...

Huyu jamaa mguzi wa rangi, kaburu wa kutupwa!

Anonymous said...

Duh...jamaa si mtaalamu wa mambo ya baolojia wala saikolojia. Kwa kutujua tu TEKNOHAMA, keshanjiona anaweza kutafuta kujua Waafrika wana akili kiasi gani!!!????

Makubwa haya!!!!!!

Akiachwa Kalahari mwenyewe, hafikishi siku 3 atakufa na akili zake akiwaacha wazawa wakidunda!

Hivi vigezo vya IQ watu wenye busara waliviacha siku nyingi kwa sababu havitoi picha halisi ya binadamu.

Anataka kutwambia kuwa Waafrika wote, waishio barani Afrika na waishio mabara mengine wote wajinga?

Wanorwejiani wote na wazungu wote duniani hata wavuta bwimbwi wote wana akili kuliko Waafrika?

Mjinga wa kutupwa!

Sijui anaishi karne ipi?

Mzee Tambaza said...

MWACHENI KAMA ALIVYO. ANATAKA WATU TUPANDISHE HASIRA ZA MKIZI, TUFANYE UJINGA HAWALAFU YEYE NA WENYE MAWAZO KAMA YEYE WASEME:

MNAONA? TUMESEMA SISI, HAO HAWANA KICHWANI KICHWANI, TUKISEMA MNATUONA WABAGUZI..

NDIVYO ANAVYOTAKA!!!