Tuesday, May 11, 2010

Norway

Wilaya ya Halden yafunga Facebook


Uongozi wa wilaya ya Halden, mkoa wa Østfold, iliyopo mpakani na Sweden, umefunga matumizi ya Facebook kwa wafanyakazi wake, baada ya kugundulika kuwa wafanyakazi wengi wa wilaya hiyo hutumia muda wao mwingi kuvinjari kwenye ukurasa mtandao  jamii huo, badala ya kufanya kazi.

Meya wa mji wa Halden, Bw. Per Kristian Dahl, ambaye ni mtumiaji mkuu wa Facebook, ameshangazwa na ufungwaji wa mtandao huo bila yeye kuwa na taarifa. Meya huyo yuko safarini nje ya nchi.

Wilaya hiyo yenye wakazi 28063, ina watumiaji karibu 10000 wa Facebook kila siku.


No comments: