TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam wanaungana na mabalozi mengine duniani kwa kutumia fomu DS -160 kwa waombaji wa viza ya matembezi ya muda mfupi. DS 160 itakuwa inapatikana kwa waomba viza Tanzania kuanzia tarehe 03-05-2010 na itakuwa ni lazima kwa kila muomba viza kuanzia tarehe Mei 31, 2010. Kila muomba viza anashauriwa kuanza kutumia fomu hii mpya bila kuchelewa.
Idara ya Uhamiaji, Wizara ya mambo ya nje Marekani imeboresha DS-160kwa wale waombaji wa viza ya muda mfupi (NIV) Fomu hii italeta mabadiliko kwenye fomu zote zinazopatikana kwenye mtandao (EVAF) Mabadiliko haya yataleta mabadiliko kwenye hatua ya kwanza ya maombi ya Viza. DS-160Ina faida nyingi kwa waombaji wa viza Dar es Salaam ambao tayari wameisha jaza fomu zao kupitia kwenye mtandao.
Tofauti ya fomu hii mpya waombaji wa viza watatakiwa kutuma maombi yao ya viza kupitia mtandao. Waombaji wa viza wanatakiwa kuhifadhi fomu zao kwa matumizi ya siku zijazo. Unatakiwa kutuma picha ya mnato, na kama maombi yanakuwa ni ya kundi unashauriwa kutumia fomu itakayokuwa ya vikundi ili kuepuka makosa ambayo yanaweza kujitokeza wakati wa kujaza.DS-160 itahitaji kila muomba viza kujibu maswali yote ili kuepusha usumbufu ambao ubalozi itabidi wakurudishe kutokana na kutokamilika kwa fomu zako.
Uchunguzi uliofanywa na huduma kwa wateja Duniani umeonyesha mafanikio makubwa ya kuridhisha na fomu hii mpya. Muombaji viza atatakiwa kuleta uthibitisho wa kupokelewa kwa maombi yake Ubalozini wakati wa mahojiano. DS -160 inapatikana kwenye mtandao na maelekezo ya hatua yatakuwa yanapatikana kupitia tovuti yetuhttp://tanzania.usembassy.gov kuanzia 03-05-2010 Waombaji viza ya matembezi ya muda mfupi kwa sasa wanajipangia muda (miadi) Fomu mpya ya DS-160 Haitabadilisha utaratibu wa kujipangia miadi. Waomba visa wataendelea na utaratibu wa kujipangia miadi kwa mahojiano ya viza. Miadi inapatikana kwenye tovuti http://tanzania.usembassy.gov Muombaji anatakiwa kuleta uthibitisho wa maombi yake, picha na nyaraka.
Ili kupata DS-160 fomu, tafadhali fungua hapahttp://ceac.state.gov/genniv/. Kwa maelezo zaidi, tafadhalia tembelea tovuti yetu U.S Embassy Dar es Salaam http://tanzania.usembassy.gov au wasiliana na idara ya uhamiaji kwa barua pepe drsniv@state.gov
No comments:
Post a Comment