Saturday, May 29, 2010

Tanzania

Usalama magari ya Rais utata mtupu




UTATA umeibuka kuhusu usalama wa magari anayotumia Rais Kikwete kufuatia tukio linalohusisha magari  aliyotumia wakati wa ziara yake ya jiji la Dar es Salaam ya Jumatatu wiki hii ambapo moja lilipata matatizo ya tairi na jingine kuzima ghafla.

Wakati wa ziara hiyo, gari alilopakia Rais Kikwete lilizimika katika makutano ya barabara ya Morogoro na Mavurunza, wilayani Kinondoni, eneo la Kimara Mwisho, saa 7:30 mchana, na hivyo kusababisha msafara wake kusimama kwa dakika tatu.


No comments: