Friday, May 14, 2010

Uingereza yapiga marufuku noti za Euro 500


Mabenki na Bureau de Charge nchini Uingereza yamesimamisha ununuaji na uuzaji wa noti za Euro 500,- baada ya kugundulika kuwa zinatumiwa na wahalifu na mafisadi kusafirisha nje ya nchi hela nyingi zilizopatikana kwa njia isiyo halali. Kila noti ya Euro 500 ni sawa na Paundi za Kiingereza 426,-.

Kufuatilia taarifa za idara inayoshughulika na uhalifu wa mali na ufisadi ya Uingereza; Serious Organised Crime Agancy (SOCA) noti hizo hazitumiki tena Uingereza.

SOCA wanasema kuwa mtu mzima anaweza kumeza Euro 150,000.00 (laki moja na hamsini elfu) na Euro 20,000.00 (ishirini elfu) zinaweza kuwekwa kwenye paketi ya sigara na kuvushwa kutoka Uingereza. Hiyo inatokana na saizi ndogo za hizo noti za Euro.  Kitu ambacho hakiwezekani kwa Paundi zenye gharama hizo.

Chanzo: SOCA.

No comments: