Friday, May 14, 2010

McDonald Sweden wauza
hambaga na saladi za zamani


Wafanyakazi wa baadhi ya mikahawa ya McDonald nchini Sweden wamekuwa wakibadili tarehe za hamba na saladi za zamani na kuziwekea tarehe mpya, huku wakijua fika kuwa kufanya hivyo ni kuhatarisha afya za wateja wao.

Stesheni ya luninga ya taifa ya Sweden (SVT) imefanya uchunguzi kwenye moja ya mikahawa ya kampuni hiyo ya ”fast food” na kugundua mchezo huo. Mfanyakazi mmoja wa mkahawa huo aliiambia stesheni hiyo ya luninga kuwa, waliambiwa na bosi wao kuwa; si ruhusa kutupa chakula.                                

No comments: