Friday, June 25, 2010

Ahadi ni duni, mbona hamchuni?



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke, 
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi Frank,

Vipi soka mpenzi wangu? Mbona timu zetu zote zinapigwa? Ila angalau wale Nyota Weusi wametuokoa kidogo. Lo hata mimi niliye mbumbumbu wa mpira ninasikitika, sijui wewe unaonaje kweli na ushabiki wako wa kukubuhu. Laiti tungekuwa wote nikuliwaze kidogo mpenzi wangu. Lakini uko mbali na mimi; hivyo nakumbatia hewa tu, kama si mto badala ya mtu. Na nikiota, nakuotea wewe ukichezea Bafana Bafana! ....bofya na endelea>>>>>


No comments: