Friday, June 25, 2010

Matangazo ya sigara



TANZANIA: Baada ya kupitishwa sheria ya kuzuia uvutaji sigara migahawani na hotelini, Serikali iliamuru kila wenye migahawa au hoteli kuweka tangazo la sheria hiyo, mambo yalikwenda kama ufuatavyo:

MATANGAZO:

Mgahawa wa Msomali: Habana kufuta dumbago habah, kama nafuta dumbago haba serkali atashkuwa hatwa mkali kabeisa.

Mwarabu: Habana kufuta mtumbatu ndani ya myumba hii, mtu ukufuta mtumbatu haba tabigwa kwa kishwa yake halafu tabelekwa kwa bolis!

Jaluo....... Ni makufuru kuvuta singara kipande ii. Kama we nakamatwa inavuta singara kipande iii tapelekwa direct kwa prison.

Mhindi....Serkali sema pana buta sigara apa. basi watu ote pana buta sigara apa!

Makonde; Hailuuchiwi kubuta chigala apa otelini. Ukibuta chigala apa utapigwa nchale na kupelekwa chelikalini!

Msukuma: Inakatazwagwa kuvutaga masigala apa. mtu akivunja hili lishelia atapelekwa kwa mwanagwa jitabu.

Mpemba. Sigara zeshakatazwa kuvutiwa humu ngahawani hivo, na msifanye nchezo, Bwan Juma ni nkali atawatia jela wabishao na atawatoa kwenye CUF!

Hoteli ya mwana CCM:  Kufatana na sababu zisizoweza kuzuilika, serikali imechukuwa hatua nyeti ya kupinga uvutaji wa sigara kidamnasi ya watu, migahawani na mahotelini. Pia imeelezwa kinagaubwaga kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka sheria hii. Wahudumiwa wote wanapaswa kuzingatia amri hii ili kuepukana na kile kinachojulikana kama mkono wa sheria.


No comments: