Tuesday, June 22, 2010

Rais Kikwete ateua mabalozi saba


Rais Jakaya Kikwete ameteuwa mabalozi saba kushika nafasi mbalimbali katika balozi zetu nchini Sweden, Canada, Ehiopia, Paris-Ufaransa na Balozi wa Kudumu Kwenye Umoja wa Mataifa.

Katika uteuzi huo Rais Kikwete amemteua
Mohamed Mwinyi Haji Mzale kuwa balozi wetu Stockholm Sweden, anachukua nafasi iliachwa wazazi na Ben Moses aliyestaafu utumishi wa Umma.

Wengine walioteuliwa ni Alexander Masinda kuwa balozi mpya Ottawa, Canada kuziba nafasi ya Peter Kallaghe aliyeteuliwa kuwa balozi wa Tanzania London. Kallaghe anachukua nafasi ya Mwanaidi Sinare Maajar ambaye mapema mwaka huu alihamishiwa Washington DC.

Aidha, aliyekuwa Balozi wa Tanzania Washngton DC, Ombeni Sefue ameteuliwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu kwenye Umoja wa Mataifa kushika nafasi iliyoachwa wazi na Augustine Mahiga ambaye ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa mwakilishi wake maalum kwenye mgogoro nchini Somalia.

Katika uteuzi huo pia aliyekuwa balozi wa Tanzania Brazil, DKT Joram Biswaro amehamishiwa Addis Ababa na Umoja wa Afrika wakati aliyekuwa Balozi Mohamed Maundi amerejehswa nchini kuwa Mkuu wa Chuo Cha Diplomasia, Dar es Salaam.

Aidha Rais Kikwete amemteau Begum KArim-Taj kuwa balozi, Paris kujaza nafasi iliyoachw awazi na Hassan Gumbo Kibelloh aliyestaafu.


No comments: