Wasauzi waaga fainali,
Ufaransa warudi kwao kwa aibu
Afrika Kusini leo imecheza kiume na kuwafunga Wafaransa kwa magoli 2 – 1 kwenye mechi iliyochezwa kwenye uwanja ”Free State Stadium”. Licha ya kuwafunga Ufaransa, Afrika Kusini wamekuwa nchi ya kwanza waandalizi wa fainali za kombe la dunia, kuyaaga mashindano kwenye raundi ya kwanza. Wameyaaga mashindano wakiwa na pointi 3. Ufaransa nayo inarudi kwao kwa aibu, kwa kuwa timu ya mwisho kwenye kundi hili, ikiambulia pointi moja tu. Kwenye mechi zingine kwenye Uruguay imeifunga Mexico 1 – 0. Kwenye kundi hili, Uruguay imekuwa ya kwanza ikifuatiwa na Mexico, ndizo timu zitakazoendelea kwenye ngwe ya pili ya fainali hizi.
Kundi B
Naijeria nayo nje!
Naijeri VS. Korea Kusini 2 – 2
Ajentina vs. Ugiriki 2 – 0
Ajentina wamechukua nafasi ya kwanza kwenye kundi hili kwa pointi 9, wakifuatiwa na Korea Kusini pointi 4. Naijeria wamekuwa wa mwisho kwa kuwa na pointi 1
No comments:
Post a Comment