Thursday, June 24, 2010

Sorry Azzure, Waitalia
Wanyang´anywa ubingwa na kutolewa


Kundi F

Timu ya taifa ya Italia (Azure) imechapwa magoli  3 – 2 na Slovakia na kuvuliwa ubingwa wa dunia waliochukua Ujerumani mwaka 2006. Kwa matokeo hayo, Italia imeshika mkia kwenye kundi F na kuziaga fainali za kombe la dunia. Kwenye mechi zingine la kundi hili, New Zealand ilitoka sare na Paraguay bila kufungana. Hivyo basi, Paraguay imekuwa mshindi kwenye kundi hili kwa pointi 5, ikifuatiwa na Slovakia kwa pointi 4, ndizo zinazoingia kwenye hatua ya michuano ya timu 16.





Kundi E

Matokeo ya kundi hili

Uholanzi vs. Kameruni  2 – 1

Japan vs. Denmarl  3 – 1

Uholanzi na Japan wanaingia kwenye duru ya kutoana ya timu 16

No comments: