Friday, June 25, 2010

Vihiyo hata Norway wapo!

Bi. Liv Løberg

Mkurugenzi mkuu wa utumishi kwenye idara inayohusika kuhakiki viwango na vyeti kwenye sekta ya afya hapa Norway, Statens autorisasjonskontor for helsepersonell, Bi. Liv Løberg amefoji vyeti vya elimu yake, amegundulika na ameachia ngazi mara moja tu ilipojulikana kuwa ni kihiyo!

  • Bachelor of Science & Economics, Queen Mary College, London (amefoji)
  • Master of Science, London School of Economics and Public Administration, University of London (amefoji)
  • Master of Public Administration, Norwegian School of Economics and Public Administration, Bergen, Norway (amefoji)

Curriculum Vitae yake kabla ya kugundulika ilikuwa inaonekana hivi; bofya na angalia (samahani iko kwa Kinorwejiani). Baada ya kugundulika inaonekana hivi; bofya na soma…


Hivi karibuni iligundulika kuwa idara hiyo, Statens autorisasjonskontor for helsepersonellimekuwa ikiidhinisha vyeti vya kutoka nje ya Norway na kuwapasisha wenye vyeti hivyo, huku wakijua kuwa wengi wenye vyeti hivyo wamevipata kwa njia ya udanganyifu huko walikotoka na kuwa vyeti vingi walivyovihakiki na kuviidhinisha ni vyeti vya kufoji. 


Sasa tunaelewa kwa nini walifanya hivyo, kwani mkuu mwenyewe naye amefoji vyeti vyake!!!

Tayari ameshafunguliwa mashtaka ya kufoji vyeti vya elimu yake.


1 comment:

Anonymous said...

Duh! Hii kali mno.

Huyu mama hakuwa hata nesi...