Friday, July 02, 2010

Hivi ni kazi ya sheria kutunyima haki?


Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


FRANK wangu,

Mwishoni imebidi nikuandikie shairi maana naona ndiyo njia pekee ya kuhimili mihemko ya michemko ya hapa.

Mpenzi wangu wa enzi,
Nipe fursa nikuenzi
Nikiwazia ujenzi
Wa maishani na mwenzi

Unapokaa mbali
Kwa kweli sina hali
Niko na wenye mali 
Lakini hawanijali

Nikuambie mpenzi
Kukaa na Wabenzi
Ni kuvumilia ushenzi 
Wa kupigwa makwenzi

Nami katu sikubali
Kupelekewa hospitali
Kwa kusema ukweli
Hata kama ni kwa kejeli



No comments: