Thursday, July 01, 2010

Tanzania

Serikali yaongeza muda wa kusajili
simu za mikononi



NA MAGRETH KINABO NA BENJAMIN SAWE MAELEZO-DODOMA

SERIKALI imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani ili kuwezesha wananchi wengi waweze kujisajili baada ` kusikiliza kilio chao ili kuwapa fursa zaidi ya kujisajili.Hayo yalisemwa jana Bungeni na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msollla wakati akiwasilisha hotuba yake ya makadrio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo. “Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu imesikia kilio cha wananchi wengi.

Imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani hadi Julai 15, mwaka huu baada ya hapo simu zote ambazo hazijasajiliwa zitafungwa,” alisema Profesa Msolla .Aidha Waziri Msolla alisema jumla ya kampuni 14 hadi sasa zimepewa leseni ya kutoa huduma za mawasiliano ya simu. Aliongeza kuwa idadi ya watumiaji wa simu kwa kigezo cha njia za simu (line) zinazotumika imefikia 18,207,390, hivyo idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 400 ikilinganishwa na watumiaji 3,542,563 waliokuwepo mwaka 2005.

Alisema idadi ya simu za mezani hadi sasa ni 174,800 ilinganishwa na 154,420 zilizokuwepo mwaka 2005. “Hii ni sawa na ongezeko la la asilimia 13.2 . ukuaji huu umepanua wigo wa mawasiliano ya simu na kuongeza huduma nyingine zinazoendana na matumizi ya simu hapa nchini Alizitaja huduma hizo kuwa ni upatikanaji wa taarifa, huduma za mtandao, ulipaji wa Ankara za simu, maji, umeme na huduma za kibenki. Awali Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa agizo kuwa namba zote za simu za mkononi zisajiliwe kati ya Julai 1, mwaka 2009 hadi Desemba 31, mwaka 2009.

Awali mamlaka hiyo iliongeza muda wa mara ya pili wa miezi sita wa kusajili simu hizo, kuanzia Januari mwaka 2010 hadi Juni mwaka huu baada ule wa kwanza kuonyesha watu wengi walikuwa hawajajisajili.

No comments: