Soko la pamoja la Afrika Mashariki
laanza rasmi leo.
TANZANIA imefungua milango ya ajira mbalimbali zikiwamo za ualimu na uuguzi kwa ajili ya raia wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) chini ya Soko la Pamoja linaloanza kutekelezwa rasmi leo.
Nchi nyingine wanachama ni Uganda, Kenya, Rwanda, na Burundi ambazo pia zimeainisha ajira ambazo hazitakuwa na vikwazo kwa raia wa nchi mwanachama kuzipata katika nchi husika.
“Raia wa nchi wanachama wataruhusiwa kutafuta ajira katika maeneo yaliyofunguliwa katika nchi mwanachama yeyote na kutobaguliwa kwa misingi ya utaifa, katika masuala ya ajira na maslahi na haki nyingine za mfanyakazi,” amesema Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax.
Ajira zilizofunguliwa na Tanzania kwenye sekta binafsi kwa nchi wanachama bila kubanwa na sheria ya kazi inayokataza kuajiri wageni kwenye maeneo ambayo watanzania wanamudu, ni pamoja na ualimu wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu, maofisa ugani, wauguzi na wakunga, waongoza ndege, wahandisi wa fani mbalimbali na upimaji ramani.
Akifafanua jana maeneo ya msingi yaliyoondolewa vikwazo chini ya itifaki ya Soko la Pamoja, Tax alisema walimu wa vyuo vikuu wanaoruhusiwa kuanzia sasa kufanya kazi nchini ni wenye Shahada za Uzamivu.
Walimu wa sekondari walioruhusiwa ni wenye Shahada katika masomo ya Sayansi, Hisabati na lugha za kigeni na utekelezaji wake umepangwa kuanza mwaka 2015.
Kwa upande wa shule za msingi, kuanzia mwaka huu wanaruhusiwa walimu wa kutoka nchi wanachama wenye shahada za kwanza na wengine wanaoruhusiwa kuingia nchini kuanzia mwaka huu ni wa kilimo, ufundi stadi na utamaduni.
Ajira nyingine zilizoruhusiwa wageni kutoka nchi wanachama kuzipata na mwaka wa utekelezaji kwenye mabano ni maofisa ugani (2015), wauguzi na wakunga (2010), waongoza ndege (2012) na upimaji ramani (2015).
Kwa upande wa Kenya, miongoni mwa ajira zilizofunguliwa ni za utawala na uongozi, utaalamu katika masuala ya Sayansi, Hisabati, kompyuta, takwimu, Uhandisi na elimu maalumu.
Ajira nyingine ni kwa walimu wa shule za msingi na elimu ya juu, waongoza ndege, mawakili na maofisa wa sheria, wandishi wa habari, wafamasia, wauguzi, wasanii wa katuni, uchoraji na sanaa ya muziki.
Nchini Uganda, chini ya Soko hilo, raia wa nchi yoyote mwanachama, hana kikwazo cha kwenda kufanya kazi za uandishi wa habari, umakamu mkuu wa chuo kikuu, usanii, uanamuziki na uongozaji ndege.
Burundi imeweka wazi ajira za walimu wa vyuo vikuu, wauguzi na wakunga na wanataaluma wa Fizikia, Hisabati na Sayansi ya uhandisi kwa wageni kutoka nchi wanachama wa EAC.
Miongoni mwa ajira zilizofunguliwa Rwanda kwa ajili ya wageni ni za wataalamu wa Sayansi ya Jamii, Uhandisi, Upima ardhi, Utawala na Ualimu.
Akizungumzia uhuru wa raia wa Afrika Mashariki kuingia katika nchi yoyote ndani ya Jumuiya, Tax alisema raia atawajibika kuwa na hati halali ya kusafiria na kupita katika vituo rasmi mipakani, ambako baada ya kukamilisha taratibu za Uhamiaji, atapewa hati ya kuingia na kukaa nchini kwa miezi sita.
Hata hivyo habari kutoka Rwanda zilisema nchi zote za EAC isipokuwa Tanzania, zimeruhusu matumizi ya vitambulisho vya kitaifa kama hati halali za kusafiria. Tanzania iko katika maandalizi ya kuchapisha vitambulisho hivyo.
Kwa upande wa matumizi ya ardhi na majengo, Ibara ya 15 ya Itifaki, inasema suala hilo litasimamiwa ndani ya nchi mwanachama na sheria za nchi husika.
“Hili la ardhi ni miongoni mwa masuala yaliyoibua hisia, watu wakadhani wageni wangekuja kuchukua ardhi. Lakini tumelinda maslahi ya Tanzania, wakija wageni watawezeshwa kupata maeneo ya biashara ila wataongozwa na sheria zetu za uwekezaji na ardhi,” alisema Tax.
Majadiliano ya Itifaki ya kuanzisha Soko la Pamoja yalikamilika Oktoba mwaka jana na kufuatiwa na marais wa nchi wanachama, kuisaini Novemba 20 mwaka jana mjini Arusha.

Kutoka Habari Leo
No comments:
Post a Comment