Thursday, September 16, 2010

Duniani kuna mambo

Amuua mkewe kwa rimoti
Jamaa mmoja toka London amefikishwa mahakamani na hukumiwa kifungo cha miaka 3 jela baada ya kumuuwa mkewe kwa kumpiga na rimoti ya kichwa. Rimoti hiyo iliyo kuwa na uzito wa gramu 160 ilimpiga mkewe kichwani na kumpasua mshipa wa ndani ya ubongo. Chanzo cha tukio hilo ni baada ya wawili hao kuwa katika mabishano juu ya mtoto wa kambo wa jamaa huyo huku wote wakiwa wamelewa pombe na madawa ya kulevya.

Katika kupingana na msemo usemao wanaume kwa wanawake ni sawa na mfupa kwa fisi ndio akamua kumfyatua mkewe na kifaa hicho. Akiwa mahakamani alidai kuwa hakutarajia kama mkewe angefariki na wala hakukusudia kumuuwa ukizingatia ni rimoti ya TV.

Chanzo:
·         Daily Mail UK
·         The Times UK
·         The Guardian UK
·         This Is London

No comments: