Wednesday, September 01, 2010

Milioni 3 wasio na makaratasi nchi
za Jumuiya ya Ulaya (EU)
wapata msamaha...



Zaidi ya watu milioni tatu waliokuwa wakiishi bila ya makaratasi kwenye nchi za EU, wamesamehewa na kupewa vibali vya kuishi, kati ya mwaka 1996 hadi 2007, hiyo inafuatia ripoti toka Centre for Migration Policy Development.

Kuanzia jana kwenye jengo la ”Litteraturhuset” mjini Oslo, kumekuwa na kongamano la wadau wanaotetea wageni wanaoishi nchini Norway bila ya kuwa na vibali vya kuishi.

Kwenye kongamano hilo, Bw. Petter Eide wa Norwegian Peoples Aid (Norsk Folkehjelp), nchi kama Sweden, Uholanzi, Hispania, Ureno, Ubelgiji, waliamua kuwasamehe watu wasio na makaratasi, hivyo basi kama nchi hizo zimefanya hivyo, Norway pia inaweza kutoa msamaha kwa waishio hapa bila makaratasi.

Inasadikiwa kuwa zaidi ya watu 18000 wanaishi Norway bila ya kuwa na makaratasi na idadi inaongezeka kila kukicha.

No comments: