Tuesday, October 19, 2010


Anapata kr. 10 000,-
(T.shs. 2 519 045,-) kwa siku!!!




Kijana Erik  Storli, ambaye kawaida anafanya kazi kama muuzaji kwenye duka la chakula la Rema 1000 Sentrumgården, mjini Bodø, anapata kroner elfukumi kwa siku.

Erik ametengeza App (application) iitwayo  «iLlumination» inayotumika kwenye iPhone 3GS na iPhone 4 kama tochi. Mpaka sasa hivi Wamarekani 350 000 na Wanorwejiani zaidi ya 1000 wameifyonza na kuiweka kwenye iPhone zao.

«iLlumination» inashika namba moja kwenye Apple Store

App hiyo ni dezo kuifyonza, jamaa anapata hela kwa matangazo kwenye app hiyo. Kila ikifyonzwa, kunatokea tangazo na ndipo jamaa anapata hela.

Mchana anafanya kazi kama muuzaji dukani, usiku kijana huyo anakesha kutengeza app.

No comments: