Tuesday, October 19, 2010

Elimu haina mwisho –
Miaka 99 anafanya Ph.D 

Bholaram Das, akiwa nyumbani kwake, Gauhati nchini India. Picha na AP.


Msemo wa Waswahili kuwa elimu haina mwisho umejihidhrisha ni wa kweli. Babu Bholaram Das wa miaka 99, ametimiza miaka hiyo wikiendi iliyopita. Ametangaza kuwa amejiandikisha kama mwanafunzi wa shahada ya uzamivu (Ph.D) kwenye chuo kikuu cha Gauhati, nchini India.

Anatarajia kutafiti kuhusu dini ya Uhindi (Hinduism) kwenye kijiji chake.

Bholaram alianza kazi kwanza kama mwalimu, baadaye akasomea sheria na kuwa wakili mpaka alipostahafu mwaka 1971.


No comments: