Friday, October 08, 2010

Bulawayo, Zimbabwe


Genge la wanawake
linalobaka wanaume


Kumezuka genge la wanawake nchini Zimbabwe, linalobaka wanaume. Genge hilo limeubukia kwenye mji wa Bulawayo. Mpaka sasa wanaume watano wanadai kuwa, walitekwa na genge hilo halafu kubakwa kwa zamu na wanawake wa genge hilo kwa nyakati tofauti.

Hivi majuzi mwanamme mmoja anadai kuwa genge hilo likiwa na wanawake watatu, walimpa lifti, akiwa kwenye gari, walimziba pua kwa nguvu na kitambaa chenye nusu kaputi. Alipokuja kushtuka akakuta yuko wa mnyama na wanawake hao wakimbaka kwa zamu.

Katika matukio mengine mwezi uliopita; wanaume wawili walitekwa kwa nguvu na wanawake hao wakabakwa  wakiwa na akili zao timamu, huku wameshikiliwa bastola na mmoja wa wanawake hao.

Msemaji wa polisi wa Bulawayo, Bw. Wayne Bvudzijena anasema kuwa, mpaka sasa hawaelewi sababu za genge kubaka wanaume, lakini kuna hisia miongoni mwa wakazi wa Bulawayo kuwa ni  sababu za kishirikina. Mpaka sasa hivi hakuna sheria yoyote inayokataza wanawake kubaka wanaume nchini Zimbabwe.


1 comment:

Anonymous said...

Nitahamia Bulawayo! Ukame utaniisha