Tunawafundisha nini watoto wetu jamani? Ni mzazi wa Kitanzania, anatundika picha ya mwanae hewani hivi ili walimwengu waone jinsi aleavyo mwanae.
Huyu mtoto hajui afanyalo na akikua kwa maadili haya, mzazi atakuwa na haki ya kumkea mtoto kama huyu?
Hivi ile Sheria ya Watoto (The Children Act, 2009) ina maana yeyote kwa Watanzania kama ilivyo kwa wenzetu Ulaya na Marekani ?
Tokea imetungwa mwaka Jana 2009, sijapata kusikia makali yake hata kidogo japo ilisemekana itazuia mambo kama haya ikiwemo kupiga vita tabia za wazazi kuwatuma watoto baa au kuingia nao Baa na kumbi za starehe .
Mdau Ngoshwe
1 comment:
Hii si sawa kabisa..mengi sina!!!
Post a Comment