Friday, October 08, 2010

Faini ya Dala milioni 873,-
(Kroner 5,200,000,000,-)
kwa kueneza ”spam” zenye
picha za nanihii na bangi
kwenye facebook.


Juzi mahakama ya Quebec nchini Canada (Quebec Superior Court) imehitimisha hukumu aliyopewa Adam Guerbuez mwaka 2008, kwa kueneza “Spam” halaiki zenye picha za nyeti za kiume na bangi kwenye Facebook.

Mwaka 2008 Guerbuez alihukumiwa na mahakama moja nchini Marekani, kulipa Dala za Kimarekani milioni 873,- (sawa na Kroner za Kinorwejiani 5,200,000,000,-) kwa kitendo chake cha kuiba nywila (koda/password) kibao za watumiaji wa facebook na kueneza “spam” kwenye facebook. Pia amehukumiwa kutotumia tena facebook katika maisha yake.

Guerbuez anajigamba kuwa hatalipa hata senti tano kwa vile amejitangaza kuwa amefilisika na kwa sheria Marekani na Canada, mtu aliyejitangaza kuwa ni muflisi halipi deni alilokuwa anadaiwa.

Guerbuez bado anatwita: http://twitter.com/adamguerbuez


1 comment:

Anonymous said...

Duh! Faini hii hata tungepigwa Tanzania tungefilisika!!!!!!!!!!!!!