Wakazi wenye asili ya kigeni
waishi kwa kiwewe!
Wiki nzima hii, wakazi wa Malmø wenye asili ya kigeni wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi, baada ya kutokea mtu ambaye hajulikani kuwavizia na kuwapiga risasi za kushadidia miale (leza au kwa Kiingereza “laser”) kwa kutumia bastola. Mpaka sasa watu zaidi ya 17 wamepigwa risasi na kudra za Mungu mpaka sasa hapajatokea maafa ya kifo, zaidi ya baadhi ya waliopigwa kupatwa na majeraha. Polisi wa Malmø wameunda kikosi maalumu cha maofisa 50 wa msako wa usiku na mchana kumsaka mtu huyu, hadi sasa hawajafanikiwa. Jana polisi wa Malmø walimkamata mtu mmoja wa miaka 50, wakamhoji kwa masaa kadhaa kwa kumshuku kwa matukio haya, lakini baadaye walimwachia.
Baadhi ya wakazi wenye asili ya kigeni, wameanza kuingiwa na kiwewe na hata kukataza watoto wao kwenda shule na wenyewe kukaa nyumbani kwa kuhofia maisha yao!
Hii inaonekana ni marudio ya matukio kama haya yaliyotokea Malmø kwenye miaka ya 90 na mtu mmoja kuuawa. Mpaka sasa mtu aliyefanya kitendo hiki, hajakamatwa.
Polisi wana wasiwasi kuwa mtu huyu aidha hapendi watu wenye asili ya kigeni, punguani au ni mtu anayetaka kujulikana tu kwa kufanya vitendo hivi.
Malmø ni mji wa tatu wa ukubwa baada ya Stockholm na Gothenburg.
Kwa habari zaidi fuatilia kwenye: http://www.thelocal.se/
No comments:
Post a Comment