Tuesday, October 26, 2010

Malmø, Sweden

Majambazi yaliyostahafu yamwinda
mpiga bastola wa leza

Genge moja la majambazi waliostahafu mjini Malmø, limesema kuwa limeanza msako wa kumtafuta mtu ambaye amekuwa akipiga watu risasi za leza na mpaka sasa hivi amewalenga na kuwapiga risasi watu 20 wenye asili ya kigeni mjini humo.

Mmoja wa kinara wa genge hilo aliyekataa jina lake kutajwa ameliambia gazeti moja la Malmø; Sydsvenska kuwa - Ole huyo jamaa wakimkamata kabla ya polisi - watamvunja miguu asiweze tena kutembea maishani mwake.

Genge hilo limesema kuwa polisi wameshindwa kazi na kuwa wao wanakifahamu fika kitongoji cha Rosengård kinachokaliwa na wakazi wengi wenye asili ya kigeni mjini Malmø. Hivyo basi itakuwa rahisi kwao kumkamata huyo mtu kabla ya polisi wa Malmø.

Inspekta wa polisi wa makosa ya jinai; Bw.Börje Sjöholm anawasihi wakazi wa waachie vyombo vinavyohusika kufanya kazi zao na kuwa wasijichukulie sheria mkononi.

Watu maarufu wenye asili ya kigeni wanaotokea kwenye kitongoji cha Rosengård ni pamoja na wacheza mpira maarufu Zlatan Ibrahimović, Yksel Osmanovski, Labinot Harbuzi, Goran Slavkovski na "rapa" Rebstar wamezaliwa na kukulia Rosengård.

No comments: