Tuesday, October 26, 2010

Mwalimu wa kwanza kusimamishwa kufundisha
kwa maisha nchini Uingereza

Mwalimu Nisar Ahmed (46), amekuwa mwalimu wa kwanza nchini Uingereza kufungiwa kufundisha kwa maisha. Halmashauri ya waalimu Uingereza (The General Teaching Council for England) imetoa uamuzi wa kumsimamisha Mwl. Ahmed kuwa hawezi kazi ya kufundisha kwani amekuwa hana mipangilio kwenye ufundishaji wake, amekuwa akichelewa darasani, hasahihishi kazi za wanafunzi na hata akisahihisha anachelewa kuzirudisha. Mara nyingi amekuwa akisahau kazi za wanafunzi kwenye gari na mara nyingi amekuwa akiingia darasani bila kujitayarisha.

Ahmed alikuwa mkuu wa idara ya biashara kwenye John O'Gaunt Community Technology College in Hungerford, Berkshire, toka Septemba 2007 hadi Januari 2009. Amefundisha kwa miaka 13.

Toka mwaka 2000 ni waalimu 13 tu waliosimamishwa kufundisha kwa muda na baadaye kuruhusiwa kurudi kazini. Hii ni mara ya kwanza nchini Uingereza kwa mwalimu kutoruhusiwa kufundisha tena katika maisha yake.

No comments: